October 13, 2016

CHAMA (KULIA) AKIWA NA TALIB HILAL AMBAYE SASA NI KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA UFUKWENI YA OMAN. 

Mchezaji nyota wa zamani wa Yanga, Athumani Chama amezushiwa lakini mwenyewe amethibitisha si kweli.

Chama amesema kwamba bado anaumwa sana, lakini anamshukuru Mungu.

“Naumwa sana, bado naumwa. Lakini nipo namshukuru Mungu,” alisema kwa ufupi.

Mchana kutwa kwenye mitandao, suala hili lilikuwa likipita kuonyesha kwamba mkongwe huyo anayesumbuliwa na ugonjwa wa kupooza, amepoteza maisha.

Hivi karibuni, beki wa zamani wa Simba, Talib Hilal alimtembelea Chama nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. Kabla wawili hao walikuwa wapinzani wakubwa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV