October 13, 2016


Inaonekana kuna matumizi mabaya ya mitandao, kwani Msemaji wa Ruvu Shooting, naye amezushiwa kifo.

Hii imetokea baada ya taarifa kusambaa kwamba Athumani Chama, mchezaji wa zamani wa Yanga, kuwa amefariki dunia, kumbe ni uzushi mtupu.

Lakini, Masau naye amezushiwa kifo kupita mitandaoni na juhudi za kumpata zilipofanikiwa ilikuwa hivi:

SALEHJEMBE: Kaka pole, tuliingiwa hofu baada ya hizo taarifa.
MASAU: Ahsante, sijui hawa watu wanataka nini?

SALEHJEMBE: Kwa nini, unawajua walioanzisha huu uzushi?
MASAU: Hakuna ninayemjua, ila watu wanapiga simu kuniulizia na wengine wanasema wameona mitandaoni.

SALEHJEMBE: Ulikuwa mgonjwa, huenda kuna mtu akatumia hiyo njia kusambaza uzushi huo.
MASAU: Siumwi hata kucha, ndiyo maana nashangaa na nimekuwa naendelea na shughuli zangu kama kawaida.

SALEHJEMBE: Pole sana kama, tuko pamoja.

MASAU: Ahsante sana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV