October 4, 2016Hali ni mbaya katika kikosi cha Antalyaspor kinachoshiriki Ligi Kuu nchini Uturuki.


Pamoja na kuongozwa na mshambuliaji nyota wa zamani wa Real Madrid, FC Barcelona na Inter Milan, Samuel Eto’o lakini bado kinashika mkia.


Istanbul BB inaongoza ikiwa na pointi 16, wakongwe Besitas na Galatasaray wanafuatana wakiwa na pointi 14 kila mmoja huku Antalyaspor ikiwa mkiani na pointi 2 tu baada ya mechi sita.


Antalyaspor inashika mkia huku ikionekana haina matumaini ya kujikwamua chini ya nahodha Eto’o ambaye pia aliwahi kukipiga nchini England akizitumikia Chelsea na Everton kwa nyakati tofauti.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV