October 5, 2016


Kampuni namba moja katika uuzaji wa matairi ya magari nchini ya Bin Slum Tyres Ltd, imewafanyia ‘sapraiz’ vijana wa timu ya taifa ya Serengeti Boys kwa kuwajaza mamilioni.

Kampuni hiyo ambayo pia huuza betri za RB zinazoaminika kuwa namba moja kwa ubora nchini, kimyakimya iliahidi kuwapa Sh milioni 3 kama watafuzu kwenda kucheza Kombe la Mataifa Afrika na nusu yake wakishindwa. Lakini imeamua kutoa fedha zote Sh milioni 3 licha ya kwamba hazijafuzu.


Mwakilishi wa Bin Slum Tyres Ltd,  Hassan Ngua Kimazi, alikabidhi fedha hizo kwa Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime.

Lakini kwa furaha akawaita vijana wake, nao wakakabidhiwa fedha hizo pamoja huku wakionyesha furaha kubwa.

“Kwa niaba ya Mkurugenzi wetu Nassor Bin Slum, tumeona tuwajali vijana wetu. Ingawa ahadi hii ingekuwa kama wakifuzu lakini bado tunawaona ni mashujaa na waliopambana kwa ajili ya taifa.


“Hivyo wanastahili hiki tunachotoa kuonyesha tunawadhamini. Kampuni yetu ni ya Watanzania wote, hivyo tunawawakilisha katika hili kwa nia ya kuonyesha uzalendo na kuwajaza moyo vijana kama hawa kwamba hawapaswi kuvunjika moyo, bado wana safari ndefu,” alisema Hassan.

Naye Shime alisema: “Shukurani nyingi sana kwa Bin Slum, ameonyesha uzalendo na kweli hakuna kati yetu alitegemea. Ilikuwa ni ahadi ya kimyakimya, hasa tukifuzu. Lakini hatujafuzu lakini bado ametuzawadia na hii inatupa moyo kwamba wako watu wanajali kwa ajili ya taifa lao.”

Serengeti Boys ilikuwa ifuzu kwenda Madagascar, lakini kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Congo iliyokuwa ugenini, tena katika dakika ya 90+2, kilipoteza matumaini ya Watanzania wote.

Hata hivyo, vijana hao wamekuwa wakionyesha kila linalowezekana kufanya vizuri zaidi hadi walipofikia hatua hiyo.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic