October 5, 2016


Mwamuzi Martin Saanya na wasaidizi wake Samwel Mpenzu na Wasaizidi wake, Ferdnand Chacha hawajafungiwa.

Jana kulikuwa na taarifa kwamba wamefungiwa miaka miwili baada ya kuboronga mechi ya watani Yanga na Simba iliyochezwa Jumamosi iliyopita.

Lakini Kamati ya Bodi ya Ligi ya uendeshaji na Usimamizi wa Ligi iliyokaa jana, imefikia uamuzi wa kuendelea kujiridhisha kwa kuangalia ulivyokuwa uchezeshaji wao.

Uamuzi huo, maana yake watatu hao hawajewa adhabu hadi hapo kamati itakapojirisha na kutoa taarifa.

Taarifa kutoka ndani ya kamati hiyo, zimeeleza, baada ya kujiridhisha kupitia kamishna wa mechi, inaweza kurejea na kulizungumzia hilo suala.


Hata hivyo, kamati hiyo inaonekana kwenda mwendo wa kobe kuhusiana na kilichoamuliwa jana na kamati, lakini taarifa zimeanza kuzagaa kila sehemu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV