Serikali imetangaza kuzuia mchakato wa ukodishwaji na uwekezaji ndani ya klabu za Yanga na Simba.
Yanga tayari ilikuwa imemkodisha Yusuf Manji kwa miaka 10 na Simba ilikuwa katika harakati za kumuuzia hisa 51 Mohammed Dewji, sasa yote hayatafanyika,
Taarifa iliyotolewa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupitia katibu mkuu wake, Mohamed Kiganja imesitisha zoezi hilo hadi hapo klabu hizo zitakapofanya mabadiliko katika katiba zao.
Katika taarifa ya Kiganja, imesema zoezi hilo limesitishwa hadi matekebisho ya klabu zote mbili kupitia sheria ya msajili wa michezo namba 442, kanuni ya 11 kifungu kidogo cha (1-9).
Pamoja na kueleza hilo, mwishoni taarifa hiyo inaonyesha wazi kwamba serikali haitaki mchakato huo baada ya kusema mjadala umefungwa lakini inasisitiza wanaotaka kumiliki timu zao, basi wafanye juu chini kumiliki klabu zao kama alivyoamua kufanya Said Salim Bakhresa.
0 COMMENTS:
Post a Comment