October 5, 2016


PLUIJM
Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm amelitafakari bao walilofungwa na kiungo wa Simba, Shiza Kichuya kisha kuja na mtazamo wake juu ya bao hilo ambalo liliinyima timu yake pointi tatu.

Pluijm alishuhudia kikosi chake kikiambulia sare ya bao 1-1 mbele ya Simba licha ya kuongoza hadi dakika ya 87 ambapo mara baada ya mchezo huo kocha huyo amesema kutojipanga vyema kwa safu yake ya ulinzi na kuridhika na ushindi ndiyo kuliwaponza na kujikuta wakiambulia pointi moja.

Pluijm amesema, kwamba Kichuya aliweza kuifunga timu yake bao hilo kwa sababu walishindwa kujipanga sahihi katika dakika nne za mwisho ambapo waliwaruhusu wapinzani wao kupeleka mashambulizi kila walivyotaka na mwisho wake wakajikuta wanaruhusu bao hilo.

“Unajua kwamba tulifungwa mara baada ya sisi kupoteza umakini wetu katika kumaliza mchezo, hasa katika dakika zile za mwisho kwa kuona kuwa tumeshashinda tayari na kuwaruhusu wapinzani kucheza wanavyotaka na mwishowe wakaambulia sare.

“Ni uzembe ambao ulijitokeza katika safu yetu ya ulinzi kwa kushindwa kujipanga na kuzuia tukio lile mpaka mpira unaingia wavuni, naamini kama wangeongeza umakini basi wangecheza mpira ule lakini tumepata pointi moja ambayo ni nzuri kuliko kukosa kabisa japo haikuwa malengo yangu,” alisema Pluijm.

SOURCE: CHAMPIONI 


1 COMMENTS:

  1. Kitu kingine watu waache ushabk mech ya smba na yanga sio ya mchezo wala marefari hawatakiwi kuhukumiwa lasivyo mtawamalza kwa kuwafngia, na mtaleta hata wagen watashndwa tu mtaona maamuz yao sio sahihi maana sio viongoz wala watu wa kawaida ushabk mwing mno!.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV