October 5, 2016Baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Ruvu Shooting, kocha mkuu wa Azam, Mhispania, Zeben Hernandez amefunguka kuwa sababu kubwa ya matokeo hayo yanatokana na uzembe uliofanywa na wachezaji wake huku akisisitiza kamwe hataweza kuwalaumu kwa kilichotea.

Katika mchezo huo uliopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar, timu hiyo ilijikuta ikilazimishwa sare kwa bao la jioni lililofungwa na Shaban Kisiga.

Timu hiyo kila siku zinavyozidi kwenda imekuwa haina matokeo mazuri, kwani ilianza kwa kuongoza ligi lakini kwa sasa tayari imeshacheza mechi saba, imejikusanyia pointi 11 na kushika nafasi ya sita.

Zeben amesema matokeo hayo mabaya hakuna wa kulaumiwa kwani ni sehemu ya mchezo.

“Kiukweli malengo yalikuwa ni kushinda lakini kwa bahati mbaya mambo mwishoni yamekwenda tofauti na matarajio yetu, kila mtu anaelewa wapi tulipo hivi sasa kwani mambo ni magumu kiasi chake ila tutapambana.


“Lakini hakuna wa kulaumiwa kwa matokeo haya zaidi ya kuendelea kufanyia kazi makosa ili yasitokee hapo mbele kwa sababu kama kucheza muda wote tulicheza vizuri na kuongoza katika kila kitu na kilichotokea ni makosa  ya kibinadamu tu kila mtu anaelewa,” alisema Zeben.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV