October 4, 2016


Mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars dhidi ya Ethiopia iliyopangwa kufanyika Oktoba 8 mwaka huu, imeahirishwa.

Mechi hiyo iliyokuwa ichezwe mjini Addis Ababa imeahirishwa kutokana na vurugu zinazoendelea mjini humo.

Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine amesema wanaendelea na juhudi za kutafuta mechi nyingine.

“Tunachofanya kufanya juhudi za kutafuta mechi nyingine ya kirafiki katika muda huu mchache uliobaki.

“Kama itakuwa imefanikiwa, itakuwa ni jambo jema, ikishindikana basi tutamtaarifu kocha,” alisema.


Kumekuwa na machafuko nchini humo, hali iliyosababisha baadhi ya watu kuumia katika vurugu kati ya wananchi na polisi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV