October 4, 2016
Uongozi wa klabu ya Yanga, umeandika barua kuomba kuutumia Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar kwa ajili ya mechi zake za Ligi Kuu Bara na mashindano mengine.

Yanga imechukua uamuzi huo baada ya Serikali kutangaza kuifungia yenyewe pamoja na Simba kuutumia Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Serikali imetangaza kuufungia uwanja huo baada  ya vurugu za mashabiki zilizojitokeza wakati wa mechi ya watani hao.

Uamuzi huo wa Yanga kama utapita kupitia ombi lao, maana yake timu zitalazimika kusafiri kwenda Zanzibar kuifuata Yanga ambayo itakuwa nyumbani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV