November 19, 2016


Yanga wamepanga kuanza mazoezi mapema zaidi licha ya kwamba walionekana kama wamechoka.

Kikosi cha Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, wamemaliza ligi hiyo mzunguko wa kwanza wakiwa katika nafasi ya pili nyuma ya Simba kwa tofauti ya pointi mbili tu.

Uongozi wa Yanga, umeamua kikosi hicho kuanza mazoezi mapema baada ya kuwa kimetoa mapumziko hayo ya wiki mbili.

"Nafikiri siku ni zilezile, lakini mazoezi ya Yanga yataanza mapema," kilieleza chanzo.

Pia kuna taarifa, Yanga itasafiri kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kuweka kambi.

Yanga imemaliza ligi hiyo ikiwa katika kiwango kizuri tofauti na ilivyoanza kwa kusuasua.

Taarifa zimeeleza, lengo la kuanza mapema pia ni kumpa kocha George Lwandamina nafasi ya kuanza kuwanoa wachezaji wake wapya.

Hivi karibuni, Lwandamina alizungumza na SALEHJEMBE na kusema wiki mbili za mapumziko ni nyingi sana na badala yake wachezaji walipaswa kupumzika huku wakijiendeleza na michezo mingine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV