November 5, 2016Yanga ilikuwa na hofu ya kumkosa beki wa kulia, Hassan Kessy baada ya jana Ijumaa kushindwa kumaliza mazoezi ya timu yake kufuatia kupata maumivu ya mgongo na kuzua hofu ya kutocheza mechi dhidi ya Prisons.

Lakini leo asubuhi amerejea mazoezini na anaonekana kuwa fiti tayari kwa ajili ya mechi ya kesho Jumapili dhidi ya Prisons.

Prisons iliyo katika nafasi ya tisa na pointi zake 16 katika Ligi Kuu Bara, kesho itacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Sokoine katika muendelezo wa ligi hiyo.

Katika mazoezi ya Yanga jana Ijumaa asubuhi kwenye Uwanja wa Sokoine, Kessy alishindwa kumaliza mazoezi hayo na kuzua hofu ya kukosa mechi dhidi ya Prisons.

Kessy hucheza beki ya kulia akipokezana na Juma Abdul ambaye sasa ni majeruhi wa maumivu ya kiuno na misuli, hivyo nafasi hiyo kama Kessy hatakuwepo, atacheza mchezaji kiraka ambaye ni Mbuyu Twite.

Daktari wa Yanga, Edward Bavu, amesema: “Kessy amepata mshtuko mgongoni, ndiyo maana hajaendelea na mazoezi, sitegemei kuona akikosa mechi na Prisons, japokuwa itategemea na hali yake.”


Kwa upande wake, Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm akizungumzia hali hiyo ya Kessy, alisema: “Ni maumivu madogo, ila bado ana muda wa mazoezi, tutamsikiliza daktari kuhusu hali yake halafu ndipo tutamtumia.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV