November 5, 2016 Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm amesema atahakikisha timu yake inaifunga Prisons, kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Sokoine jijini hapa lakini wachezaji wa timu hiyo wameiambia Simba kamwe isijidanganye kuhusu kutwaa wa Ligi Kuu Bara ubingwa msimu huu.

Pluijm baada ya kupoteza mechi dhidi ya Mbeya City, Jumatano wiki hii kwa kufungwa mabao 2-1, amesema atahakikisha wanapata pointi tatu dhidi ya Prisons na kupunguza tofauti ya pointi kati yao na Simba.

Simba ipo kileleni mwa ligi kuu ikiwa na pointi 35 katika mechi 13 kama ilizocheza Yanga yenye pointi 22 ikiwa nafasi ya pili.

“Mambo mengi yalitokea tukapoteza dhidi ya Mbeya City, lakini hiyo haiwezi kuwa maana ya kupoteza mechi zote za Mbeya, tuna mechi na Prisons naamini tutafanya vizuri baada ya maandalizi ya uhakika.

“Tumebadilika kidogo hasa katika mbinu ili tuweze kupata pointi tatu ambazo zitapungua pointi kati yetu na timu inayoongoza, naamini itakuwa hivyo,” alisema Pluijm.


3 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Chezeni mpira, acheni kuimba taarab. Simba one at a time. Nguvu moja

    ReplyDelete
  3. Babu unaondoka kabla ya mzunguko wa kwanza kuisha. Wachezaji wako kumbe wamekuwa waimba taarab?

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV