November 16, 2016Baada ya kukimbiwa na viungo wake wawili, Mtibwa Sugar imeanza kukiboresha kikosi chake kwa kumsajili kiungo wa Malindi ya Zanzibar, Saleh Khamis.

Mtibwa kwenye usajili mkubwa wa Ligi Kuu Bara waliondokewa na viungo wao muhimu kwenye kikosi chao ambao ni Mzamiru Yassin na Mohamed Ibrahim waliotua Simba.

Tangu Mtibwa waondokewe na viungo hao wameonekana kukosa uimara kutokana na kumtegemea Ibrahim Rajab ‘Jeba’ pekee.

Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo, kiungo huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Mtibwa.

 “Kama unavyojua timu yetu kila msimu wanaondoka wachezaji na kwenda kwenye klabu kubwa za Simba na Yanga, msimu huu kama ulivyoona ameondoka Mzamiru, Mohamed na Kichuya (Shiza) ambao wote walikuwa tegemeo.

“Hivyo, tunachofanya ni kuwapata mbadala wao kwenye usajili huu wa dirisha dogo na tayari tumempata mbadala wa Mzamiru na Mohamed ambaye ni Saleh kutoka Malindi inayoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar,” alisema mtoa taarifa huyo.


Kwa upande wa Saleh alipotafutwa akasema: “Hizo taarifa ni za kweli kabisa, mimi hivi sasa ni mchezaji halali wa Mtibwa Sugar baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV