November 18, 2016Meneja wa Simba, Mussa Hassan Mgosi ameibiwa simu yake katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.

Taarifa zinaeleza, aliyeiba simu ya Mgosi amekuwa akiitumia katika masuala ya utapeli.

“Ameiba simu ya Mgosi halafu anaitumia kuwaomba watu fedha, jambo ambalo si sahihi,” alisema mmoja wa marafiki wa karibu wa Mgosi.


Bado hatujafanikiwa kumpata Mgosi lakini taarifa zinaeleza yuko katika harakati za kutoa taarifa Polisi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV