November 30, 2016



Katika siku za hivi karibuni kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ambaye mkataba wake na timu hiyo unafikia tamati mwezi Januari mwakani, alisema kuwa mpaka sasa haelewi chochote kama ataendelea kuitumikia timu hiyo au la.

Kutokana na hali hiyo, Mkude akawataka Yanga wakamsajili kama kweli wanamhitaji akidai bila kusita atasaini timu hiyo, kwani yupo tayari kuitumikia.

Jambo hilo linadaiwa kuukera uongozi wa Simba na umeamua kuchukua jukumu la kukaa kimya bila ya kumfuatilia tena kiungo huyo na wamesema kama anataka kwenda Yanga aende.

“Mkude hivi sasa anatakiwa kuwa makini sana, vinginevyo anaweza kujikuta katika wakati mgumu kwani uongozi umesema kuwa hautahangaika naye tena, yeye kama anataka kuondoka basi aondoke zake.

“Wamefikia hatua hiyo baada ya kumbembeleza sana kusaini mkataba mpya lakini yeye amekuwa akizingua akidai kuwa fedha anazotaka kupewa ni kidogo lakini pia kila akiitwa kwa ajili ya mazungumzo amekuwa akikataa,” 
kilisema chanzo chetu cha habari na kuongeza:

“Kutokana na hali hiyo uongozi wa timu unamsubiria kocha aje ili uweze kuzungumza naye na ikiwezekana aanze kuwa anamtumia Mzamiru Yassin kama kiungo mkabaji halafu Juma Awadh awe anacheza namba nane.”

Alipotafutwa Mkude ili aweze kuzungumzia hali hiyo alisema: “Kama wamefikia uamuzi huo ni wao lakini binafsi kwa sasa siwezi kusema chochote juu ya suala hilo.”


2 COMMENTS:

  1. Hasira ni hasara kwa wapinzani wetu simba juu ya kiungo wenu mkabaji Jonas Mkuda. Kaeni meza moja muelewane

    ReplyDelete
  2. Kwa mchezaji makini wa Simba kusema hadharani kama Yanga wanamtaka waje tu,ni kosa kubwa sana la kimaadili,ijapokuwa kwa sasa mpira ni pesa.Ingekuwa mie ni kiongozi wa Simba huyo mkude simba asingevaa tena jezi ya simba labda akiwa chumbani kwake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic