December 7, 2016



Kocha Mkuu wa Majimaji ya Ruvuma, Kally Ongala ameweka wazi kwamba katika kuelekea mzunguko huu wa pili wa ligi, kikosi hicho hakitacheza mchezo wowote ule wa kirafiki kwa kuogopa wachezaji wake kupata majeraha ambayo yanaweza kusababisha wasifanye vizuri kwenye mechi zao.


Ongala ambaye aliinusuru timu hiyo kutoka mkiani na kumaliza katika nafasi ya 13 wakiwa na pointi 16 wanaendelea na kambi yao mkoani humo ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi.


Ongala amesema kwamba hawatacheza mechi yoyote ya kirafiki katika kipindi hiki ambacho kimebaki muda mchache kabla ya ligi kuanza kutokana na mechi nyingi za namna hiyo wapinzani huwa wanapania kwa nia ya kutaka kushinda.


“Sisi ni tofauti na timu nyingine ambazo zinawaza kwamba zitacheza michezo ya kirafiki kwa ajili ya kujiweka imara zaidi, kwetu haitakuwa hivyo kwani tunaogopa kupata majeruhi ya wachezaji wetu haswa ukizingatia kwamba muda wenyewe umeshamalizika hivyo kama tukipata majeruhi itatuharibia mipango yetu.


“Tutakachokifanya ni kuendelea na mazoezi yetu tukiwa na lengo moja la kutaka kufanya vizuri katika mzunguko wa pili na tunaamini tutafanikiwa juu ya hilo kwa sababu tumepata muda mrefu wa kujiandaa tofauti na mzunguko wa kwanza ilivyokuwa ambapo sasa tumepata muda wa kukijenga vizuri kikosi na tutasumbua vilivyo,”alisema Ongala.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic