December 1, 2016


Kiungo mkabaji, Justice Zulu amesaini mkataba wa miaka miwili na Yanga na sasa anachoangalia ni kujiweka fiti vizuri.

Zulu amesema anachojua katika ushindani upo sehemu yoyote lakini anachotaka ni kuwa fiti ili kutoa msaada katika kikosi chake.

Zulu amemaliza na Yanga baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili tayari kuanza kazi.


Kiungo huyo ambaye hakucheza kwa zaidi ya miezi minne ndiye chaguo la kwanza la Kocha George Lwandamina tokea ajiunge na Yanga akitokea Zesco ya Zimbabwe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV