December 7, 2016



Klabu ya Coastal Union imepewa adhabu ya kucheza bila ya mashabiki kwa mechi mbili za nyumbani na mechi moja ya nyumbani kuchezwa uwanja wa ugenini kwa kosa la mashabiki wa timu hiyo kumshambulia Mwamuzi Thomas Mkombozi na kumsababishia majera ha maumivu makali.

Kama unakumbuka tukio hilo la aibu la mashabiki wa Coastal Union kumpiga mwamuzi huyo kama mwizi lilitokea kwenye UWanja wa Mkwakwani mjini Tanga katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza.

Maamuzi hayo yamefanyika baada ya Kikao cha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya Bodi ya ligi, kuwaita na kuwahoji na kuangalia mkanda wa mchezo husika. Kamati imebaini mapungufu mengi ya kiutendaji yaliyofanywa na waamuzi hao, na hivyo kuitaka kamati ya waamuzi ishughulikie.

Maana yake, kama waamuzi hao nao watakutwa na hatia kutokana na mapungufu yao, pia wataadhibiwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic