Watu takribani 10,000 wanatarajia kuingia kwenye pambano la kuwania ubingwa wa dunia wa WBO kati ya Mtanzania Francis Cheka dhidi ya mwenyeji wake Vijenda Singh.
Pambano hilo linatarajia kuchezwa Desemba 17 huku Cheka akiamini ana nafasi ya kufanya vizuri kwa kuwa ndiyo mara ya kwanza amesafiri na kocha wake, Abdallah Saleh ‘Komando’ katika safari ya nje.
Singh hajawahi kupigwa na amekuwa akifanya kazi zake za ngumi nchini Uingereza, lakini sasa amerejea kupigana katika ardhi ya nyumbani kwao.
Cheka amezungumza na SALEHJEMBE kutoka nchini India na kusema yuko tayari licha ya rekodi nzuri ya mpinzani wake.
“Kweli ana rekodi nzuri sana, lakini mimi ninataka kushinda na kuwa bondia wa kwanza kushinda dhidi yake,” alisema Cheka.







0 COMMENTS:
Post a Comment