December 21, 2016



Msanii wa hip hop anayetamba hivi sasa na wimbo wake wa Muziki, Sharrif Thabeet ‘Darassa’ amesema kuwa hataki kuamini imani za kishirikina kuhusika kwenye ajali aliyoipata huku akitamka yote hayo ni mipango ya Mungu.

Kauli hiyo, ameitoa ikiwa ni siku moja tangu anusurike kifo akiwa na ‘crew’ yake baada ya kupata ajali maeneo ya Ntobo barabara ya kuelekea Mgodi wa Bulyanhulu Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, akiwa anaelekea kwenye shoo.
Darassa alipata ajali hiyo ya gari akiwa na maprodyuza wake Remmy Raymond ‘Mr VS’, Habbar na dairekta wake Hanscana wakiwa kwenye gari aina Toyota Harrier.


Darassa amesema gari lao halikuwa spidi kiasi cha kusababisha wao wapate ajali, lakini ghafla aliona usikani ikikataa kurudi kutoka kulia kuja kushoto eneo walilokuwa wanaelekea.

“Kiukweli kabisa nikwambie tu, hakukuwa na tatizo lolote katika safari yetu, nilishangaa ghafla kuona gari lenyewe likielekea upande wa kulia na kikubwa cha kushukuru hatukuwa kwenye mwendo wa kasi.

 “Ninaamini kama ningekuwa naendesha kwa mwendo wa kasi, basi sidhani kama tungetoka kwenye ajali hii tuliyoipata na kitu kingine cha kushangaza hakukuwa na chanzo chochote cha ajali kwa maana labda mbele au nyuma yetu kulikuwa na gari lingine, tulikuwa wenyewe.

 “Mimi sitaki kuamini kama nimerogwa bali namshukuru Mungu tu,”alisema Darassa.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic