December 14, 2016



FC Barcelona imeitwanga Al Ahli ya Saudi Arabia kwa mabao 5-3 katika mechi ya kirafiki iliyomalizika hivi punde huko Doha, Qatar.
Katika mechi hiyo ya kirafi, Luiz Suarez, Lionel Messi na Neymar kila mmoja alifunga bao moja kabla ya wote watatu kutolewa katika dakika ya 32.
Kocha Luis Enrique aliwatoa wakali wake hao kwa kuwa wana mechi ngumu ya La Liga Jumapili dhidi ya Espanyol ambayo hujulikana kama Catalan Derby.

Barcelona iliongoza kadi kwa mabao 5-1 baada ya  Paco Alcacer na Rafinha kila mmoja kufunga katika kipindi cha pili.

Lakini Al Ahli nao walijitutumua na kupata mabao hayo matatu kupitia kwa Omar Abdulrahman ambaye ni mwanasoka bora wa Bara la Asia,  na Muhannad Assir aliyepiga bao mbili.


Barcelona ilitua Qatar jana, leo imecheza mechi na baada ya hapo, wachezaji wake wameingia kwenye ndege kurejea Barcelona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic