Kiungo Mghana anayeaminika amekuja kujiunga na Simba
kuziba nafasi ya Jonas Mkude, ametua nchini.
James Kotei ametua nchini leo saa 10:50 jioni
akitokea kwao Ghana tayari kumalizana na Simba.
Mchezaji huyo kinda, anasifika zaidi kwa ukabaji na
utoaji wa pasi ndefu anatarajia kumalizana na kusaini mkataba na Simba, kesho
kwa kuwa mazungumzo ya awali yalishakamilika.
Mratibu wa Simba, Abbas Ally 'Dizzo' ndiye aliyejitokeza kumpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kusema kwamba, baada ya mazungumzo ya mwisho kati yake na klabu hiyo kongwe, taarifa itatolewa.
Acha uchonganishi mkuu, alie kwambia mkude anaondoka simba nani, mnatumia vibaya dhana ya chanzo chetu cha kuaminika
ReplyDelete