Kiungo wa Yanga, Mzambia, Justine Zulu, ametamka kwamba apewe muda wa kuendelea kuzoea mazingira mapya ndani ya timu hiyo kabla ya kuonyesha uwezo wake ambao ulimfanya awe chaguo la kwanza la usajili wa kocha George Lwandamina.
Zulu aliyetua Yanga kuchukua nafasi ya Mnyarwanda, Mbuyu Twite, aliyeachwa hivi karibuni, amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia timu hiyo akitokea Zesco ya kwao Zambia.
Kiungo huyo amesema kuwa licha ya kuonyesha uwezo wa kawaida kwenye mchezo dhidi ya JKU juzi, bado ana matumaini ya kufanya vizuri kwenye mechi zijazo kwani ndiyo mechi yake ya kwanza akiwa na kikosi hicho.
“Unajua kuwa ndiyo mara ya kwanza naanza kucheza na wenzangu hapa Yanga tangu nitue, toafuti na ilivyokuwa kwenye mazoezi hivyo siwezi kuonyesha uwezo mkubwa kama watu walivyofikiria kwa sababu bado sijayashika vizuri mazingira na mbinu ambazo zinatumika.
“Kwangu naona nimecheza vizuri lakini wanipe muda zaidi wa kuendelea kuisoma mienendo ya Yanga na baada ya kuelewa tu niwahakikishie kwamba nitakuja kuuwasha moto kwa kuonyesha kiwango zaidi ya hiki cha sasa,” alisema Zulu.
SOURCE: CHAMPIONI







0 COMMENTS:
Post a Comment