December 21, 2016

SALIM (MWENYE KOFIA) AKIWANGOZA WACHEZAJI WA SIMBA KATIKA MAZOEZI. HII ILIKUWA KABLA HAJAONDOKA SIMBA.


Klabu ya Simba imempa mkataba wa mwaka mmoja Kocha wake mpya wa makipa, Iddi Salim.

Salim raia wa Kenya ni mara ya pili anainoa Simba, alikuwa kocha wa makipa wakati Mwingereza Dylan Kerr akiwa kocha mkuu.

Wakati uongozi wa Simba ulipoamua kumtupia virago Kerr, ukamuunganisha kocha huyo wa makipa.


Safari hii amerejea Simba akiwa amejifua zaidi na kupata leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa), maana yake anaweza kufanya kazi nchini humo.


Salim aliwahi kufanya kazi Gor Mahia, AFC Leopards za Kenya pamoja na timu ya taifa ya nchini hiyo, Harambee Stars.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic