December 13, 2016



Klabu ya Simba imemsajili mshambuliaji nyota wa Stand United anayejulikana kwa jina la  Pastory Athanas.

Athanas amesaini mkataba wa miaka miwili leo mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva.
Kocha Joseph Omog raia wa Cameroon, mara baada ya mzunguko wa kwanza kwisha, kwenye ripoti yake aliutaka uongozi kumsajili mshambuliaji mkali atakayesaidiana na Laudit Mavugo raia wa Burundi na Frederci Blagnon.


Athanas ambaye ana umri wa miaka 22 kama ilivyoelezwa ni mmoja wa washambuliaji hatari walioshiriki Ligi Daraja la Kwanza na imeelezwa alifanya vema katika misimu miwili iliyopita.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic