January 2, 2017



Baada ya kukaa langoni kwa dakika 270 ambazo ni sawa na mechi tatu bila ya kufungwa, mlinda mlango wa Simba, Daniel Agyei, raia wa Ghana, amesema kuwa lengo lake ni kucheza zaidi ya mechi hizo bila ya kuruhusu wavu wake kutikiswa.

Agyei aliyesajiliwa na Simba katika usajili wa dirisha dogo akitokea Medeama ya nyumbani kwao, amekuja kuchukua nafasi ya Muivory Coast, Vincent Angban aliyefungashiwa virago huku akibakiwa na miezi sita kwenye mkataba wake kabla ya kumalizika.

Angban, kabla ya kufungashiwa virago, alicheza mechi kumi bila ya wavu wake kutikiswa ambapo Agyei amepanga kuzipita na kuandika rekodi mpya.

Agyei alisema anajua washambuliaji wengi wa Ligi Kuu Bara wana njaa ya kuzifumania nyavu, lakini amejipanga kukabiliana nao kuhakikisha anatimiza malengo yake hayo ikiwezekana amalize msimu bila ya kufungwa.

“Ni kweli nimeanza vizuri, kikubwa namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kwa hilo, lakini niseme tu hii si kazi yangu peke yangu bali mabeki wangu pia wanatakiwa kupongezwa kwa kunilinda vizuri.

“Matarajio yangu ni kucheza zaidi ya hapa bila ya kufungwa na ikiwezekana nimalize msimu nikiwa sijaruhusu bao, kama ikitokea hivyo itakuwa imeniongezea kitu katika ‘CV’ yangu, lakini kikubwa zaidi nataka nishinde ubingwa nikiwa na Simba,” alisema Agyei.


Simba imebakiwa na michezo 12 kabla ya kumaliza msimu huu huku ikiwa kileleni na pointi 44.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic