January 8, 2017
Jina la 4G ndiyo limegeuka kuwa gumzo katika mitandao mashabiki wa Simba wakiwakebehi watani wao Yanga.

Yanga imepoteza kwa mabao 4-0 dhidi ya Azam FC katika mechi ya mwisho ya Kundi B katika michuano ya Mapinduzi.

Mashabiki wengi wamekuwa wakiwabeza Yanga wakitumia neno la 4G ya Azam FC, wakilinganisha na ule mfumo wenye kasi wa internet wa 4G.


Mashabiki wengi wa Yanga wanaonekana kutokuwa wapole huku wengi wakiwa wametahayari kutokana na kipigo hicho kikali kutoka kwa Azam FC kwa kuwa hawakuwa wamekitarajia hata kidogo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV