January 7, 2017Kiungo wa Yanga, Deus Kaseke amesema hana tatizo na nafasi atakayopangwa uwanjani na kocha wake, kwani anamudu kucheza popote pale na kuisaidia timu.

Katika mechi mbili za Yanga za Kombe la Mapinduzi, Kocha George Lwandamina amekuwa akimtumia Kaseke kama kiungo mshambuliaji mara mbili akichukua nafasi ya Haruna Niyonzima.

Kabla ya hapo, Kaseke alikuwa akitumika kama winga wa kulia au kushoto kulingana na mahitaji ya timu kwa wakati huo lakini sasa mambo yamebadilika.

Kaseke amesema kuwa, hana tatizo na nafasi anayochezeshwa sasa kwani kokote anakocheza anaamini anafiti ndiyo maana kocha anamtumia.

“Sioni tatizo kucheza nafasi mpya kama hii ninayocheza sasa, kocha ana imani na mimi sitaki kumuangusha najua nina kazi ya kupambana zaidi ili kujihakikishia nafasi kikosi cha kwanza,” alisema Kaseke.

Leo Jumamosi Kaseke anatarajiwa kuichezea Yanga dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Kundi B wa michuano hiyo saa 2:30 usiku kwenye Uwanja wa Amaan.


3 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. Wachambuzi wa soka wanasema kwamba mchezaji mzuri unamjua pale anapokua HANA MPIRA na hili ukitaka ushahidi wake uliza wachezaji ambao wameenda kufanyiwa majaribio na kupewa mrejesho; wengi huenda kukamia na kufuata mpira kila uendako ili waonekane wanajituma lakini ukweli ni KWAMBA MPIRA HUCHEZWA KWA NAFASI NA MPIRA UNA NJIA ZAKE (ni wachezaji wachache sana wenye nidhamu katika hili hapa Bongo) ..........Moreover, Football is about team work na Kaseke ni mmoja wa wachezaji ambao kwa bahati mbaya sana hajaonekana katika hili, Kaseke ni moja ya nguzo kubwa sana Yanga anayecheza kwa nafasi na anayeshika haraka sana maelekezo ya Mwalimu, lakini kwa kuwa watanzania tunataka mpira wa anaoanao basi Kaseke huenda asikubalike sana kwa timu zetu hizi na tayari nimeanza kusikia taa nyekundu ya miguno toka kwa washabiki jambo linaloonekana kumtoa mchezoni.......KIFUPI NISEME TU HILI NDILO PAFU LA YANGA KWA SASA na nakubaliana na makocha wanaompa nafasi kwani huwa anatimiza majukumu yake barabara ambapo unahitaji jicho la kisoka kuyaona

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV