January 4, 2017Kampuni ya Yanga Yetu Ltd, ambayo iliikodisha nembo na timu ya Yanga kabla ya zengwe kuibuka, imemtimua mtendaji wake mkuu, Jerome Dufourg.

Dufourg raia wa Ufaransa ametimuliwa kazi baada ya kuonekana utendaji wake uko chini. Aliajiri Novemba, mwaka jana akitokea kwao Ufaransa.

Taarifa zinaelezwa mtendaji huyo tayari amekabidhiwa barua ya kuachishwa kazi.

Siku tatu zilizopita, gazeti la Championi liliandika taarifa za Yanga kuanchana na Mfaransa huyo.

Lakini taarifa nyingine zimeeleza, alikabidhiwa barua yake jana au leo na tayari anajiandaa kurejea kwao.


Yote hiyo, imetokana na utendaji wake kuonekana kutokuwa katika kiwango sahihi ambacho Yanga ilikuwa ikikitaji kwa ajili ya kufanya mambo yasonge kwa weledi zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV