January 11, 2017




Katika kuhakisha wanafanikisha shoo msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platinum' kwenye ufunguzi wa Afcon, Kampuni ya Multichoice kupitia king'amuzi cha DStv imetoa tiketi sita kwa vijana wake watakaokwenda nchini Gabon katika ufunguzi huo.

Ufunguzi huo wa michuano hiyo mikubwa Afrika, inatarajiwa kufanyika Januari 14, mwaka nchini huko ambako Dimaond amealikwa kwenda kutuimbuza.



DIAMOND

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alimkabidhi bendera ya taifa, Diamond kwa ajili ya kwenda kuipeperusha vyema Tanzania katika ufunguzi huo.


"Kikuweli nimpongeze Diamond kwa mwaliko alioupata wa kwenda kutumbuiza kwenye michuano mikubwa Afrika ya Afcon, siyo kitu kidogo kwake, ni nafasi ya yeye kujitangaza zaidi kimataifa, ninaamini wapo wasanii wengi wazuri Afrika, lakini kachaguliwa yeye hivyo anastaili pongezi," alisema Nape.

Nape ndiye aliwaomba DStv kujitokeza na kudhamini safari ya wachezaji shoo wa Diamond na baadhi ya watu wa timu yake kwenda Afcon ili kuhakikisha anafanya shoo ya uhakika zaidi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DStv, Salum Salum alisema wametoa tiketi hizo kwa Diamond kwa lengo kukuza na kuendeleza vema tasnia ya filamu.

"Tunathamini tasnia ya sanaa nchini kwa kupitia muziki na filamu, hivyo basi katika kutambua hilo tumetoa tiketi sita kwa kundi la WCB chini ya msanii Dimaond kwa ajili ya kwenda kwenye uzunduzi wa Afcon huko Gabon.

WAZIRI NAPE

"Tumempatia tiketi hizo, baada ya kuomba udhamini wa tiketi hizo kwa ajili ya vijana wake sita atakaombatana nao kwenye shoo hiyo na kikubwa tunataka kuona Diamond anafunika ili atauwakirishe vema," alisema Salum.

DStv, ndiyo itaonyesha michuano hiyo mikubwa ya kimataifa kwa kifurushi chake cha bei cha chini kabisa kitakachopatikana kwa Shilingi 19, 975 tu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic