January 11, 2017Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa tangu alipofanikiwa kumsajili mlinda mlango, Juma Kaseja mambo yamebadilika katika kikosi chake hicho ambapo hivi sasa kila mchezaji anataka mafanikio.


Kaseja alijiunga na Kagera Sugar hivi karibuni katika dirisha dogo la usajili akitokea Mbeya City ambako aliamua kuondoka baada ya kushindwana na uongozi wa klabu hiyo.


 Maxime amesema kuwa tangu Kaseja atue klabuni hapo mambo yamebadilika kwani amekuwa ni kiongozi na mfano wa kuigwa na wachezaji wenzake jambo ambalo linachochea morali ya mafanikio kwa kila mchezaji.


Alisema kutokana na hali hiyo anaamini kuwa kikosi chake hicho kitafanya vizuri katika mechi zake za ligi kuu zilizobakia hivyo kumaliza ligi hiyo kwa kushika moja kati ya nafasi tatu za juu.


“Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu ya mechi zetu za ligi kuu zilizobaki baada ya ligi kusimama hivi karibuni kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi, lakini napenda kumpongeza Juma Kaseja ushauri mzuri anaoutoka kwa wachezaji wangu hususani wale chipukizi.“Tangu atue hapa mambo yamebadilika kila mchezaji hivi sasa ana uchu mkubwa wa kufanikiwa jambo ambalo naamini litatusaidia kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi zetu zote zilizobakia,” alisema Maxime ambaye msimu uliopita alikuwa akikufundisha kikosi cha Mtibwa Sugar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV