January 6, 2017



Huku kikosi cha Simba kikiendelea kupambana katika Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, mshambuliaji wa timu hiyo raia wa Ivory Coast, Frederick Blagnon, anatarajiwa kujiunga na kikosi hicho leo hii akitoka jijini Dar es Salaam.

Blagnon ambaye analipwa mshahara mkubwa zaidi klabuni hapo kuliko wachezaji wengine wote, hakuambatana na kikosi hicho kwenda Zanzibar kwa ajili ya michuano hiyo kutokana na kuwa majeruhi, hali iliyofanya abakie Dar aendelee na matibabu.

Akizungumzia suala hilo, Meneja wa Simba, Musa Mgosi, alisema: “Wakati tunakuja huku, tulimwacha Blagnon kutokana na kuwa majeruhi lakini hivi sasa hali yake ni nzuri, baada ya kupatiwa matibabu ya kifundo cha mguu alichoumia katika mechi yetu ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda FC.

“Tunatarajia kuwa kesho (leo) ataungana na kikosi chetu kwa ajili ya kuiongezea nguvu safu yetu ya ushambuliaji katika michuano hii.” 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic