January 6, 2017Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi ameweka wazi kuwa wao hawana hofu hata kidogo na wapinzani wao, Azam ambao wanatarajiwa kuwavaa katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi, kesho Jumamosi.

Yanga wanakutana na Azam kwenye mchezo wa Kundi B katika Kombe la Mapinduzi wakiwa na pointi sita wakati Azam wana pointi nne, mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

“Hatutaki masihara kwa sasa na kila mchezo kwetu tunauchukulia kwa uzito mkubwa tukiwa na lengo moja tu la kupata pointi tatu na siyo jambo lingine.

“Tunawajua Azam kwamba wamekuwa wakitupa upinzani wanapokutana na sisi lakini kwa safari hii niwaambie kwamba wasahau hilo kwani tunataka kushinda na kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi.

“Kila mmoja amejiandaa vya kutosha kuona kwamba tunashinda kwa namna yoyote ile katika mechi hiyo na hilo tunaliweza kwa sababu sasa tuko katika kiwango cha hali ya juu sana na kwa kila mchezo wetu cha kwanza ni kufikiria pointi tatu na siyo kingine,” alisema Mwambusi na kuongeza:


“Tumeingia kwenye mashindano kushindana, hivyo hakuna sababu ya kuifikiria timu moja wala kusema tuna mkwepa fulani, kikubwa timu zote tunaziheshimu na zote zina upinzani,” alisema Mwambusi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV