January 12, 2017


CHECHE


Kocha wa muda wa Azam FC, Iddi Cheche amesema dawa ya Simba katika mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi iko tayari, bado kunyweshwa tu.

Simba itashuka dimbani Amaan kuivaa Azam FC katika mechi ya Kombe la Mapinduzi.

Cheche amesema maandalizi yanakwenda vizuri na Simba, haiwezi kumpa hofu.

"Imebaki kuwanywesha tu dawa yao, nimecheza na Simba wakati nikiwa mchezaji. Najua aina yao ya uchezaji, kawaida huwa haibadiliki sana.

"Naweza kusema dawa yao imekamilika na kila kitu kitakwenda vizuri," alisema.

Azam FC ambayo ilianza michuano hiyo kwa kusuasua, iliitwanga Yanga kwa mabao 4-0 katika mechi ya mwisho ya makundi na kutinga nusu fainali kwa kishindo.

Hali hiyo inaonyesha kuamsha hali ya kujiamini kwa Azam FC ambayo siku chache uongozi wake uliwatimua makocha kutoka Hispania.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV