January 12, 2017Simba huenda ikamkosa kiungo wake mshambuliaji Mohammed Ibrahim katika mechi ya fainali, kesho.

Simba itashuka dimbani Amaan kuivaa Azam FC katika mechi ya Kombe la Mapinduzi.

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema bado hali ya Mo Ibrahim haijaimalika kwa asilimia mia.

“Kila kitu kinakwenda vizuri na maandalizi ni mazuri. Lakini Ibrahim, hali yake bado si asilimia mia. Hivyo ni suala la kuendelea kuangalia,” alisema.

Mo Ibrahim alilazimika kutoka nje na nafasi yake kuchukuliwa na Laudit Mavugo katika mechi ya nusu fainali dhidi  Yanga. Simba ilishinda mechi hiyo kwa mikwaju ya penalti 4-2.

Mayanja alisema Simba inatambua mechi hiyo ni ngumu na itapambana vilivyo kuhakikisha inafanikiwa kubeba ubingwa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV