January 11, 2017


Beki Juma Abdul wa Yanga ndiye amekuwa gumzo zaidi mitandaoni kutokana na kuonyesha ubabe wake.

Abdul anaonekana kwenye picha akijaribu kumkaba beki wa Simba, Abdi Banda licha ya kwamba ana umbo kubwa kuliko yeye.

Beki huyo wa Yanga, alivaana na Banda wakati wa mechi hiyo ya watani hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, jana.

Vurugu lilianza baada ya Banda kumuangusha Kaseke ambaye alionekana kuumizwa kutokana na hali hiyo, Abdul akamvaa Banda na kuanza kumvinya usoni.

Hata hivyo, baadaye mwamuzi wa mchezo huo aliwaramba kadi za njano wote wawili kwa hatua hiyo.

Ukiangalia inaonekana Abdul ana umbo sana ukimlinganisha na Banda. Lakini inaonekana hakujali na alitaka kuonyesha yeye ni ‘msela’ wa Tandale na hataki mchezo hata kidogo.


Mechi hiyo iliisha kwa suluhu ndani ya dakika 90. Mwisho Simba ikashinda kwa mikwaju 4-2 ya penalti na kusonga fainali.

2 COMMENTS:

  1. hao ndio waandishi wetu wanashabikia mambo yasioyo na msingi Abdi Banda akisoma hii habari mechi ijayo atataka kulipiza kisasi na juma abdul atafikiri kucheza ubabe ni sifa hii makala ilitakiwa kuonya utovu wa nidhamu wa juma abdul badala ya kuisifia

    ReplyDelete
  2. Ni kweli kabisa hili jambo sio la kusifia...hapa jembe sikuungi mkono

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV