January 11, 2017Winga hatari wa Yanga, Edibily Lunyamila amesema kikosi cha Yanga dhidi ya Simba, kilimkosa Donald Ngoma kama pacha wa Amissi Tambwe.

Watani hao walivaana katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, jana. Simba ilishinda mikwaju 4-2 ya penalti.

Lunyamila anaamini iwapo Ngoma raia wa Zimbabwe angecheza katika mechi hiyo, basi mechi hiyo ingeisha ndani ya dakika 90.

"Ngoma angesaidia kuamua matokeo ya mechi. Beki ya Simba haikuwa makini sana, haikuwa na mtu wa kuwasumbua sana," alisema.

Ngoma anajulikana kwa usumbufu wa hali ya juu usiowapumzisha mabeki wa timu pinzani lakini ana uwezo wa kufunga pia.

Ngoma ni majeruhi na katika mechi hiyo nafasi yake ilichukuliwa na Deus Kaseke huku Tambwe akicheza namba kumi.

Hata hivyo, Tambwe alishindwa kuonyesha cheche kutokana na Simba kujaza viungo wengi na kukaba zaidi.

Hata hivyo, Yanga ndiyo ilipoteza nafasi nyingi zaidi za kufunga katika mechi hiyo.


4 COMMENTS:

 1. Marehemu asingeenda Zanzibar asingekufa..... Non sense. So simba nao wangempanga Ajib magoli yangepatikana mapema.

  ReplyDelete
 2. simba wangempanga Julko ngoma sijui angepitia wapi lunyamila anazungumza kama sio mwanamichezo

  ReplyDelete
 3. Huna point ya msingi LUNYAMILA.. Endelea na maisha mengine mpira huuwezi.. Umemuona Ngoma tu. hata cc angecheza Ajib unadhani ingekuwaje? None sense

  ReplyDelete
 4. Lunyamila,ana uchungu wa kufungwa tu,hata angecheza yeye Yanga wangeshinda tu

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV