January 29, 2017


MPIRA UMEKWISHAAA
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 89, Dida anatoka na kuidaka vizuri krosi ya Nonga ambaye aliuwahi mpira pembeni
DK 86, Yanga wanaendelea kulisakama zaidi lango la Mwadui

GOOOOOOOOO Dk 83, Chirwa anawachambua mabeki wa Mwadui na kuandika bao la pili hapa
KADI Dk 82, Tambwe analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda
SUB DK 81 Yanga wanamtoa Tambwe anaingia Said Juma
Dk 78 sasa, Mwadui wanaonekana angalau kulishambulia lango la Yanga. Lakini hakuna mashambulizi makali yanayoweza kuwatikisa Yanga
Dk 75, Salum Khamis anapiga shuti la kwanza langoni mwa Yanga lakini Dida anadaka kwa ulaini kabisa hapa
Dk 72, mpira umesimama, mwamuzi wa akiba anatibiwa hapa
Dk 70, Yanga wanaingia tena na kulisakama lango la Mwadui, MSuva aanachia shuti tena, Kado anaokoa
GOOOOOOOOOOOOO Dk 69, Chirwa anaiandika Yanga bao safi hapa baada ya shuti la Msuva, Kado akatema na yeye akaunganisha


Dk 68, Msuvaa anaachia kombora hapa lakini juuuuu
Dk 67, mpira wa adhabu wa Juma Abdul ndani ya eneo la hatari la Mwadui lakini Kadoanafanya kazi ya ziada
KADI Dk 67, mara baada ya kuanguka, Chollo analambwa kadi ya njano
Dk 65, Chollo anamuangusha Martin hapa na wote wako wanatibiwa hapa
SUB Dk 63 Yanga wanamtoa Haruna na nafasi yake inachukuliwa na Chirwa
Dk 62, Yanga wanalisakama lango la MWadui, shuti kali la Kamusoko, wanaokoa Mwadui haoa
Dk 57 Msuva anaingia vizuri tena, anaachia shuti kali hapa, goal kick
DK 56, krosi safi ya Msuva, Cholo anatokea na kuokoa hapa


Dk 54 Mwadui wanashambulia hapa lakini wanaamua kurudi nyuma huku Yanga wakiwa wachache mbele, mashabiki wanazomea hapa
SUB Dk 52 Kaseke anakwenda benchi nafasi inachukuliwa na Emmanuel Martin
Dk 50 Yondani anautoa mpira nje na MWadui wanapata kona
KADI 49 Mwamuzi Jonesia Lukyaa anamlamba kanavalo kadi ya njano kwa kucheza kindava
Dk 45, Yanga wanaanza kwa kasi, wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Mwadui. Goal kick

MAPUMZIKO
-Msuva anaachia mkwaju mkali hapa, Kado anapangua vizuri inakuwa kona hapa. Hata hivyo haina matunda

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 45, Yondani analazimika kupiga kichwa akiokoa krosi ya Kabunda. Kona ya pili kwa Mwadui, Kona ya Seseme, Dida anadaka kwa ulaini
Dk 44 sasa, Mwadui wanaendelea kugongeana vizuri lakini katikati ya uwanja
Dk 42, Dida anatoka nje na kuutoa mpira, inakuwa konaa ya kwanza ya Mwadui FC
Dk 41, Malika tena anaokoa mpira na kuwa kona. Inachongwa, Kamusoko anaunganisha shuti kali lakini goal kick
Dk 40, Malika anafanya kazi ya ziada kuokoa krosi ya Msuva, inazaa kona hapa. Yanga wanaichonga lakini haina faida
KADI Dk 37, kadi ya kwanza ya njano, Aiye wa Mwadui FC anazawadiwa baada ya kumfanyia madhambi Yondani
Dk 35, bado mpira unachezwa katikati ya uwanja zaidi
Dk 31, Mustappha anatoa mpira nje, inakuwa kona langoni kwa Mwadui FC


Dk 26, Kado anafanya kazi ya ziada, anaruka na kuudaka mpira wa Zulu
DK 20 sasa, Mwadui FC wanaonekana wamejipanga kujilinda sana na mashambulizi ya kushitukiza
Dk 20, Nonga anaingia vizuri hapa lakini Mwinyi analazimika kumuangusha
Dk 16, Mwadui FC wanaonekana wakiwa wametulia, angalau wanagonga hata pasi tano. Lakini Yanga wanaendelea kufika langoni mwa Mwadui FC
Dk 12, Kado yuko chini akipatiwa matibabu
Dk 10, Mwadui wanafanya kazi ya ziada kuokoa, inakuwa kona na Yanga wanapiga. Hakuna kitu
Dk ya 8, Kado anafanya kazi ya ziada kuudaka mkwaju wa Msuva. yanga wanaendelea kushambulia kwa kasi


Dk 7, Msuva anaingia vizuri na kumtengenezea Tambwe lakini anaachia shuti kuuubwaaa
Dk 5, Msuva anauwahi mpira wa krosi ya Juma Adul lakini anashindwa kulenga lango
Dk 4, krosi maridadi ya Mwinyi Haji lakini Kado anaruka juu na kupangua
DK 2, Awadhi Juma anaachia mkwaju mkali lakini hakulenga lango
Dk ya 1 Mechi imeanza Mwadui wakianza kusukuma mashambulizi ingawa, lakini Yanga wanakuwa wa kwanza kufika kwa Mwadui na kipa Shabani Kado anaondosha hatari

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV