January 30, 2017Straika wa Simba, Juma Luizio, amesema kikosi chao kina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kwa madai kuwa wapinzani wao ambao ni Yanga, wana michezo mingi migumu iliyobaki ukilinganisha na wao.

Simba ilipoteza mchezo wa tatu wa ligi kuu mbele ya Azam FC kwa bao 1-0 na kuwafanya wabaki na pointi zao 45, kabla ya mchezo wa Yanga jana dhidi ya Mwadui vijana hao wa Jangwani walikuwa na alama 43.

Akizungumza Luizio aliyejiunga na Simba akitokea Zesco ya Zambia, alisema hakuna sababu ya kuiondoa Simba kwenye mbio za ubingwa kwani wao wamebakiwa na michezo laini ukilinganisha na wapinzani wao Yanga ambao amedai wana mechi nyingi ngumu.

“Nafasi bado kubwa, kwa sababu bado mechi nyingi, nahisi hatuna presha yoyote, bado pointi mbili (dhidi ya Yanga ambayo ilicheza jana) huwezi jua, wenzetu wana mechi nyingi halafu ngumu ukitofautisha na sisi ngumu tushacheza, kwa hiyo naamini ubingwa upo palepale,” alisema Luizio aliyecheza mchezo wa juzi na baadaye kutolewa nafasi yake ikachukuliwa na Laudit Mavugo.   

Kauli hiyo ya Luizio iliungwa mkono na ya kocha wake msaidizi, Mganda, Jackson Mayanja, ambaye amesema: “Mashabiki wa Simba wala wasiwe na hofu ya ubingwa, licha ya kupoteza mechi na Azam kwani bado mechi nyingi zimebaki za ligi kuu kwetu na kwa wapinzani wetu Yanga tunaouwania ubingwa huo.

"Matokeo hayo yasiwakatishe tamaa, ninaamini bado tuna nafasi kubwa ya kuuchukua ubingwa huo, kikubwa tunachotakiwa ni kuendelea kupambana ili kuhakikisha tunaendelea kukaa kileleni.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV