January 29, 2017


Baada ya kipigo cha bao 1-0, mashabiki wa Simba wamelalamika kuwa washambuliaji wao ndiyo tatizo kuu.

Simba imepoteza mechi yake ya kwanza katika mzunguko wa pili kwa kuchapwa bao 1-0 na Azam FC ikiwa imefunga Simba mara mbili mfululizo ndani ya wiki mbili. Mara ya kwanza ilikuwa mjini Zanzibar kwenye fainali Kombe la Mapinduzi.


Mashabiki hao wametuma maoni yao kwenye Salehkubwa@gmail.com na kusema kuna kila sababu ya washambulizi wa Simba kubadilika.

Wengine wamesisitiza kuwa Simba haikuwa makini wakati wa dirisha dogo kufanya usajili sahihi wa washambulizi.

Hata hivyo, kumekuwa na malumbano tofauti, wengine wakisema uongozi ulifanya kila unaloweza kwa kuwa mshambuliaji kama Laudit Mavugo na baadaye Juma Liuzio walikuwa na kila sababu ya kuisaidia Simba, lakini wao ndiyo wameshindwa.


Mashabiki hao walilalamika kikosi chao kucheza pasi nyingi zisizokuwa na manufaa huku wakiishia kupata sare au kufungwa katika mechi zake za hivi karibuni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV