Simba imegoma kucheza na mabingwa wa Afrika, Mamelodi Sundowns.
Taarifa kutoka ndani ya Simba, zimeeleza uongozi wa Simba haukuwa umepata raarifa kiofisi.
Awali ilielezwa Mamelodi wangecheza na Simba kesho, mechi ya kirafiki ambayo ilipangwa kupigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
“Tumeambiwa hakuna mechi, hivyo tutaendelea na mazoezi,” kilieleza chanzo kutoka ndani ya Simba.
Tayari Mamelodi wametua nchini jana kwa ajili ya mechi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment