January 28, 2017
Yanga tangu itoke Zanzibar kushiriki Kombe la Mapinduzi imecheza mechi moja tu ya Ligi Kuu Bara na Majimaji FC ya Songea na kufunga bao moja lililofungwa na Deus Kaseke, Simon Msuva amesema akianza kufunga tena ni mbele kwa mbele hadi atakapotwaa ufungaji bora.

Msuva hadi sasa ana mabao tisa katika ligi kuu sawa na Amissi Tambwe anayecheza naye Yanga na Shiza Kichuya wa Simba, lakini tangu mwaka huu uanze hajafunga bao lolote katika ligi hiyo.

 Msuva amesema anajipanga vilivyo kuhakikisha anafunga kuanzia mechi ya kesho dhidi ya Mwadui FC na kuanzia hapo atafunga mfululizo hadi atakapotwaa tuzo ya ufungaji bora.


Msuva alisema; “Sasa tunaanza kucheza mechi zetu kwenye Uwanja wa Taifa, siyo siri nitafunga mabao mengi si unajua tangu mwaka uanze huu katika ligi sijafunga! Nitapambana kuhakikisha nafunga.


 “Timu yangu ina ushirikiano mkubwa sana katika kutafuta mabao, isipokuwa tumekuwa tukishindwa kuendana na kasi ya ufungaji kutokana na matatizo ya uwanja lakini sasa tutapata mabao. “Furaha yangu itaongezeka sana tukianza kucheza Uwanja wa Taifa, na kuonyesha furaha hiyo nitafunga mabao kila siku kiasi cha kutangaza rasmi nafasi ya ufungaji bora msimu huu kuwa ni yangu,” alisema Msuva.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV