Sasa ni uhakika kwamba Simba itamkosa
kiungo mshambuliaji wake, Mohammed Ibrahim katika mechi dhidi ya Azam FC.
Mo Ibrahim aliumia katika mechi ya nusu
fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Yanga.
Lakini akarejea mazoezini na kuanza na
kujifua na wenzake, lakini juzi alijitonesha tena kifundo cha mguu.
Kutokana na hali hiyo, ataikosa mechi ya
kesho wakati Simba inaivaa Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment