January 8, 2017


Mavugo
Mwamuzi anamaliza mchezo, Simba inatoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-0 na kusonga hatua ya nusu fainali ya michuano hii.
 
Dakika ya 90 + 2: Simba wanalishambulia lango la Jang'ombe mara mbili mfululizo.
 
Dakika ya 90: Timu zote zinashambuliana kwa zamu.
 
Dakika ya 89: Mnyate anacheza faulo nje ya 18, Jang'ombe wanapata faulo wanaipiga lakini Simba wanaokoa.
 
Dakika ya 85: Jang'ombe wanapata kona nyingine lakini inakuwa haina faida mpira unatoka nje.
 
Dakika ya 83: Kipa wa Simba, Manyika anafanya kazi nzuri kwa kuupangua mpira mara mbili baada ya Jang'ombe kupata kona iliyopigw akiufundi.
 
Dakika ya 78: Simba wanafanya mabadiliko, anaingia Vincent, anatoka Bokungu.

Dakika ya 73: Simba wanamtoa Kichuya, anaingia Hija Ugando.

Dakika ya 70: Jang'ombe wanakosa nafasi ya wazi ya kufunga, Makame anapata nafasi ya kupiga shuti akiwa mbele ya lango la Simba, anapiga shuti kali lakini linatoka nje ya uwanja.
 
Dakika ya 68: Simba wanaendelea kasi hasa kutokea pembeni.

Dakika ya 65: Zimbwe jr anapiga shuti kutoka katibu na katikati ya uwanja lakini kipa anaupangua na kuwa kona.
 
Dakika ya 62: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Juma Luizio, anaingia Kitandu.
 
Dakika ya 60: Shangwe zinaendelea kwa mashabiki wa Simba uwanjani hapa, Jang'ombe wanaendelea kuonyesha hawajakata tamaa na wanapambana.
 
Dakika ya 56: Mashabiki wanampigia makofi Mavugo kwa kazi nzuri aliyoifanya.
 

Dakika ya 55: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Mavugo anaingia, Jamal Mnyate.
 
Mavugo alipata pasi nzuri kutoka katikati ya uwanja, akaubinua mpira kwa kisigino, akaondoka nao kisha kuutengeneza mpira na kupiga shuti kali lililojaa wavuni moja kwa moja.
 
Dakika ya 54: Mavugo anaipatia Simba bao la pili shuti kali.

GOOOOOOOOOOOO!!!!!!
 
Dakika ya 48: Mashabiki wa Simba wanashangilia kuonyesha kujiamini, kumbuka kuwa kama Simba itashinda mchezo huu basi itakutana na Yanga katika hatua inayofuata.

Dakika ya 46: Jipindi cha pili kimeanza.

Timu zinaingia uwanjani kwa ajili ya kipindi cha pili.
 

Dakika 45: Kipindi cha kwanza kimekamilika, timu zomeenda vyumbani kupumzika Simba wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0.
 

Dakika ya 43: Luizio anachezewa faulo kwa kupigwa katika kifundo cha mguu, mchezo umesimama kwa muda akipatiwa matibabu.

Dakika ya 37: Mchezo unaendelea lakini kasi imepungua kiasi kwa kuwa Jang'ombe nao wanaongeza kasi.

Dakika ya 34: Beki wa Simba Mohammed Hussein anachezewa faulo upande wa kushoto, analala chini na mchezo unasimama kwa muda ili apatiwe matibabu.

Dakika ya 30: Bado Simba inamiliki mpira muda mwingi zaidi ya wapinzani wao, idadi ya mashabiki imeongezeka tofauti na mechi za Simba zilizopita kwenye uwanja huu wa Amaani, Unguja.
 

Dakika ya 27: Mavugo anaonyesha kujiamini, anamtoka beki kwa kumpiga kanzu ya kisigino lakini anashindwa kuuwahi ili kutoa krosi.

Dakika ya 22: Simba wanaendelea kujipanga na kutengeneza mashambulizi kupitia pembeni.

Dakika ya 18: Kasi ya mchezo inaongezeka. Simba wanaonekana kuwa na haraka ya kutaba bao lingine mapema.

Dakika ya 15: Simba wanalishambulia lango la wapinzani wao kwa kasi.

Luizio alikimbia na mpira upande wa kulia, akatoa pasi kwa Kichuya ambaye aliwapiga chenga mabeki kadhaa wa Jang'ome kisha kupiga shuti kali ambalo lilimpita kipa na kwenda kuambaa kwenye mstari wa goli, Mavugo akaumalizia mpira wavuni.
 

Laudit Mavugo anaipatia Simba bao la kwanza dakika ya 11 baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Luizio na Kichuya.

GOOOOOOOOOO!!!!! MAVUGOOOOOOO!!!

Dakika ya 7: Taifa Jang'ombe wanaonekana kutulia na kupiga pasi nzuri zinazoonyesha wamejipanga vizuri kutoa upinzani kwa Simba.

Dakika ya 5: Simba wanaongeza kasi muda unavyozidi kusonga mbele.
 

Dakika ya 2: Mchezo umeanza kwa mwendo wa kawaida, timu zote zinaonekana zikisomana.

Mchezo umeanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV