January 9, 2017

Kampuni ya Star Media Tanzania Limited inayouza Ving’amuzi vya StarTimes, leo Jumatatu imefungua duka lake maeneo ya Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

Mshindi, Mahmoud Mahsein Hassan (kushoto) akiwa na Juma Suluhu.

Ofisa Uhusiano na Meneja Masoko wa Star Media Tanzania Limited, Juma Suluhu amesema lengo la kufungua tawi hilo maeneo hayo ni kwa ajili ya kuwafikia zaidi wateja wao waliokuwa nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
 

“Tunataka kila kona ya Tanzania tuwe tunapatikana kirahisi, hivyo kuanzia leo wakazi wa maeneo haya na yaliyo jirani wakifika hapa watakuwa wakipata huduma zetu kirahisi na kutatuliwa matatizo yao yoyote yanayowakabili yanayohusiana na huduma zetu,” alisema Suluhu.

Naye Meneja wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Henry Ngailo, amesema tawi hilo lililopo mkabala na Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live, litakuwa wazi siku zote za wiki ambapo litafunguliwa kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 12: jioni kasoro Jumapili ambapo litafunguliwa saa 4:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni.

Aidha katika uzinduzi wa tawi hilo, kampuni hiyo ilitumia fursa hiyo kumkabidhi zawadi ya luninga mshindi wao wa Shindano la Shinda Luninga na StarTimes, Mahmoud Mahsein Hassan, mkazi wa Chamazi jijini Dar.

Shindano hilo ambalo linatarajiwa kufikia tamati keshokutwa Jumatano, limedumu kwa takribani wiki nne ambapo wateja wa StarTimes walikuwa wakiulizwa maswali mbalimbali na atakayejibu kwa ufasaha anaibuka mshindi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV