Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua
Salum Mayanga kuwa kocha wa muda (Interim coach), wa timu ya taifa ‘Taifa
Stars’.
Kocha Salum Mayanga anachukua nafasi ya Kocha Charles
Boniface Mkwasa ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi Machi, mwaka huu -
2017.
Kati ya majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha
timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON)
2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.
Pia Kocha Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi
cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa
wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).
TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa
utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 na kumtakia mafanikio katika
mipango yake inayofuata.
0 COMMENTS:
Post a Comment