January 11, 2017Hii imezoeleka mpambano kati ya timu hasimu za Simba na Yanga zinapokutana kunakuwa na vitendo vya kishirikina vinakuwa vinafanywa uwanjani lakini kwenye mechi ya jana baina ya timu hizo visiwani Zanzibar hakukuwepo na vitendo hivyo.

Unajua ilikuaje soma hapa: uwanjawa Amaan ulipofanyika mchezo huo umekuwa ukitumiwa na jeshi la Zanzibar kwa ajili ya kufanyia mazoezi kuanzia asubuhi hadi alasiri kwa ajili ya kujiandaa na sherehe za Mapinduzi ambazo zitafanyika kesho Alhamisi.

Pale uwanjani hapo liliwashuhudia makomandoo wa timu hizo wakiwa wanahaha kuzama ndani na kufanya mambo yao lakini wanajeshi waliokuwa wanafanya mazoezi uwanjani hapo hawakuruhusu mtu yeyote asiye mwana usalama kuingia ndani ya uwanja huo hadi saa tisa walipoziruhusu timu za Taifa ya Jang’ombe na Azam.


Kutokana na hali hiyo makomandoo hao walilazimika kukaa nje na juhudi zao za kutaka kufanya vitendo vya kishirikina vikakwama huku wengine wakionakana kuwasiliana kwa simu mara kwa mara.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV