February 10, 2017
Baada ya Klabu ya Simba kuondokewa na aliyekuwa katibu wao mkuu, Patrick Kahemele, rais wa klabu hiyo, Evans Aveva, ametuliza ‘mzuka’ kwa waliokuwa wakihusishwa kuchukua nafasi hiyo baada ya kusema mchakato wa kumpata katibu mpya utaanza hivi karibuni.


Mwishoni mwa mwezi uliopita, Kahemele aliachana na Simba na kujiunga na Kituo cha Runinga cha Azam TV, huku nyuma nafasi yake ikihusishwa kutakiwa na mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’.


Akizungumza jijini Dar es Salaam, Aveva amesema ni kweli kwa sasa hawana katibu mkuu baada ya kuondoka kwa Kahemele, lakini bado wamekuwa kimya kidogo na wataendelea kuwa hivyo mpaka pale muda utakapofika ndiyo watamuweka wazi mrithi wake.“Bado zoezi hilo hatujalianza lakini muda ukifika tutawatangazia ni nani atakuwa katibu wetu mpya, jambo hili halitakiwi kuamuliwa kwa haraka kutokana na nafasi yenyewe ilivyo nyeti,” alisema Aveva.

SOURCE: CHAMPIONI 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV