February 10, 2017

MTIBWA SUGAR

Kocha wa timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro, Zuberi Katwila, amefungukia juu ya kichapo cha mabao 5-0 walichokipata hivi karibuni dhidi ya Mbao FC ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kirumba, Mwanza.

Kikosi hicho kilichokuwa kinanolewa na Kocha Salum Mayanga ambaye ameteuliwa kuwa Kocha wa Taifa Stars, kilikumbana na kipigo hicho ambacho kiliwachanganya benchi la ufundi la timu hiyo kwa kuwa timu hiyo ni kongwe zaidi ya Mbao na ina uzoefu wa mechi kubwa za Tanzania.

Akizungumza Katwila alisema kuwa kipigo hicho kilikuwa halali kwao kwani refa alichezesha vizuri na hakuna hata bao moja ambalo lilipatikana kwa manzingira tata lakini kwao kilikuwa ni cha ajabu.

MBAO FC


“Hakuna jambo ambalo sitalisahau kwenye maisha yangu ya mpira kama hicho kichapo, tena ukizingatia kwa timu yetu hii kongwe kuliko wale Mbao, mimi naona kama miujiza maana yeyote kati yetu ukimuuliza kiufundi hakuna anayeweza kukueleza juu ya kufungwa huko.

“Kiukweli tulipoteza mechi yetu ile kwani siwezi kusingizia jambo lolote, refa alifuata sheria zote na kwamba wenyewe tulicheza kadiri ya uwezo wetu lakini kila tulivyokuwa tukipambana ndivyo tulijikuta tukifungwa tu,” alisema Katwila.

Kwa sasa Mtibwa wanashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 31 wakati Mbao ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 26.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV